Real Madrid hali sio nzuri,
waambulia sare dhidiya Real Betis
"Klabu ya Real Madrid ya Hispania usiku wa jumapili ya January 24 walishuka dimbani kutafuta poitnt tatu katika dimba la ugenini kucheza na Real Betis, kwa sasa Real Madrid inaendelea kuongozwa na Zidane kama kocha mkuu wa timu hiyo baada ya Rafael Benitez kutimuliwa.Licha ya kuwa Benitez alitimuliwa kutoka na uongozi wa Real Madrid kutoridhika na utendaji kazi wake na mwenendo wa timu, chini ya Zidane Real Madrid bado hajafanikiwa kuwa na uhakika wa kupata matokeo mazuri kwa kila mechi.Ikiwa katika dimba la ugenini kucheza dhidi ya Real Betis, imeambulia sare ya 1-1 na kuzidi kutengeneza utofauti mkubwa wa point na wapinzani wao FC Barcelona, Madridwalinusurika kupoteza mchezo huo, baada ya Real Betis kupata goli la uongozi dakika ya 7 kupitia kwa Alvaro Cejudo, goli ambalo Karim Benzema alisawazisha dakika 19 kabla ya mchezo kumalizika.

No comments:
Post a Comment