CHEKI NA MIMI KUPITIA

Monday, January 25, 2016



Kumekuwa na uvumi mkubwa kuwa Idris Sultan na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi na pengine very soon wawili hao watamkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza! Kama wewe ni miongoni ya watu wanaompenda Idris ama Wema Sepetu basi utapenda kufahamu aliyoyasema mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan kuhusu Wema Sepetu.
Kupitia page yake ya Instagram @Idris Sutlan, Idris kafunguka na kusema haya kuhusu Wema….
 Mimi na wewe sio kama watu wengine. Nalala, nakula na naamka nikiwa nakufikiria wewe. Unafikiri una bahati ya kuwa na mimi ila hapana mimi ndio mwenye bahati ya kuwa na wewe. Mara ya kwanza ilikuwa ajabu kwangu kuangalia ndani ya kabat langu la nguo na kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia “Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wakike” au ukiingia jikoni kwangu na kuitawala nyumba yangu na vyakula vizuri. Jinsi unavyowatazama wanawake wengine wakinisogelea, jinsi vila unavyojua ni wakati gani nahitaji a kiss au kumbatio zito. Jinsi unavyonilazimisha kuangalia channel ya Disney, jinsi unavyoniamsha mapema siku hizi kunitengenezea chai. Naweza nikakuletea ua zuri la waridi lakini halitaweza kufikia uzuri wako. Ukiwa na wivu unasonya sonya, nikiwa na wivu nataabasamu. Naweza kufanya lolote hata kuhamisha milimia kwa ajli yako. Nitakulinda, nitakupenda, nitakudekeza, nitakupikia, nitagombana na wewe, tutaangalia movies pamoja, nitakaa na wewe kuangalia nyota. Wewe ni zaidi ya kile nilichokiomba, wewe ni kila kitu changu (alisema idris)

No comments:

Post a Comment