CHEKI NA MIMI KUPITIA

Tuesday, August 11, 2015


Hatimaye Pedro Rodriguez amechukua uamuzi huu kuhusu uhamisho wake.

 Pedro mwenye asili ya visiwa vya Canary, amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United, na usiku wa leo kocha Luis Enrique alimuweka benchi huku mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Robert Fernandez amekiambia kituo cha Esport 3 kwamba Pedro ameomba kuhama.

“Pedro amenitaarifu rasmi kwamba anataka kuondoka, ila kwa sasa bado hatujapata ofa. Ikiwa kuna klabu inayomtaka basi itabidi walipe fedha ya kuweza kuvunja mkataba wake ambayo ni £21m.”
  Klabu ya Manchester United inaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya kina na Barcelona na muda wowote kutoka sasa inatarajiwa wataafikiana juu ya uhamisho huo.

No comments:

Post a Comment